Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hanania
1 Mambo ya Nyakati 25 : 4
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;
1 Mambo ya Nyakati 25 : 23
23 ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
2 Mambo ya Nyakati 26 : 11
11 Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, kulingana na hesabu walivyohesabu na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa makamanda wa mfalme.
Yeremia 36 : 12
12 akashuka, akaingia katika nyumba ya mfalme, katika chumba cha mwandishi, na, tazama, wakuu wote wameketi humo, nao ni hawa, Elishama, mwandishi, na Delaya, mwana wa Shemaya, na Elnathani, mwana wa Akbori, na Gemaria, mwana wa Shafani, na Sedekia, mwana wa Hanania, na wakuu wote.
Yeremia 37 : 13
13 Naye alipokuwa katika lango la Benyamini, mkuu wa walinzi alikuwapo, jina lake Iriya, mwana wa Shelemia, mwana wa Hanania; akamkamata Yeremia, nabii, akisema, Unakwenda kujiunga na Wakaldayo.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 19
19 Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa dada yao;
1 Mambo ya Nyakati 3 : 21
21 Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.[1]
Ezra 10 : 28
28 Na wa wazawa wa Bebai; Yehohanani, na Hanania, na Zakai, na Athlai.
Nehemia 3 : 8
8 ④ Na baada yao akajenga Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.
Nehemia 3 : 30
30 Baada yake wakajenga Hanania, mwana wa Shelemia, na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, sehemu nyingine. Baada yake akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, sehemu nyingine kuelekea chumba chake.
Nehemia 7 : 2
2 ⑫ ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Leave a Reply