Biblia inasema nini kuhusu Hanani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hanani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hanani

1 Mambo ya Nyakati 25 : 4
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

1 Mambo ya Nyakati 25 : 25
25 ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

2 Mambo ya Nyakati 16 : 7
7 Wakati huo Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea BWANA, Mungu wako, kwa hiyo limekutoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako.

1 Wafalme 16 : 1
1 Ndipo neno la BWANA likamjia Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, kusema,

1 Wafalme 16 : 7
7 Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.

2 Mambo ya Nyakati 19 : 2
2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.

2 Mambo ya Nyakati 20 : 34
34 ⑬ Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika salua ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 16 : 7
7 Wakati huo Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea BWANA, Mungu wako, kwa hiyo limekutoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako.

Ezra 10 : 20
20 Na wa wazawa wa Imeri; Hanani, na Zebadia.

Nehemia 1 : 2
2 Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliosalimika, ambao hawakuchukuliwa uhamishoni na habari za Yerusalemu.

Nehemia 7 : 2
2 ⑫ ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.

Nehemia 12 : 36
36 ⑳ na ndugu zake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, na Hanani, wenye vinanda vya Daudi mtu wa Mungu; Ezra, mwandishi, akawatangulia;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *