Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hamu
Zaburi 37 : 4
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.
Yeremia 29 : 13
13 ⑦ Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
Mathayo 5 : 6
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Mithali 2 : 3 – 5
3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu.
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Maombolezo 3 : 26
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.
1 Wakorintho 10 : 13
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
Maombolezo 3 : 25
25 BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Mithali 8 : 34
34 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Mithali 4 : 27
27 Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.
Zaburi 119 : 10
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
Zaburi 40 : 8
8 ⑱ Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Zaburi 119 : 20
20 Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu zako kila wakati.
Zaburi 37 : 7
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Zaburi 119 : 40
40 Tazama, nimeyatamani mausia yako, Unihuishe kwa haki yako.
Leave a Reply