Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia haki
1 Yohana 2 : 29
29 ④ Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
1 Petro 5 : 10
10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.
Zaburi 106 : 3
3 Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.
Yakobo 1 : 4
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Warumi 5 : 1 – 5
1 ⑮ Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
2 ⑯ ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
3 ⑰ Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira;
4 na kazi ya subira ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
5 ⑱ na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Mithali 2 : 5 – 20
5 Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu.
6 Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
7 Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;
8 Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.
9 Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema.
10 Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;
11 Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi.
12 Ili kukuokoa na njia ya uovu, Na watu wanenao yaliyopotoka;
13 Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza;
14 Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu;
15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.
16 Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;
17 Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake.
18 Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
19 Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima.
20 Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki.
1 Petro 3 : 14
14 Lakini hata mkiteswa kwa sababu ya kutenda haki, mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
1 Yohana 3 : 7
7 ⑪ Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki;
Mathayo 5 : 20
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Wafilipi 1 : 11
11 akiwa mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
Isaya 33 : 15 – 17
15 Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
17 Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.
2 Timotheo 2 : 22
22 ④ Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Yohana 3 : 21
21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
Warumi 8 : 4 – 6
4 ⑱ ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
6 ⑲ Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
2 Wathesalonike 1 : 3 – 5
3 Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
4 Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
5 Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
Warumi 10 : 4
4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Malaki 3 : 3
3 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki.
Marko 11 : 24
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
1 Wakorintho 1 : 30
30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Warumi 5 : 17
17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
Leave a Reply