Biblia inasema nini kuhusu Habili – Mistari yote ya Biblia kuhusu Habili

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Habili

Mwanzo 4 : 15
15 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

Mwanzo 4 : 25
25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.

Mathayo 23 : 35
35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

Luka 11 : 51
51 tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.

Waraka kwa Waebrania 11 : 4
4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Waraka kwa Waebrania 12 : 24
24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

1 Yohana 3 : 12
12 ⑮ si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

1 Samweli 6 : 18
18 na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale wakuu watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la BWANA, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *