Biblia inasema nini kuhusu Giza – Mistari yote ya Biblia kuhusu Giza

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Giza

Mwanzo 1 : 2
2 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Ayubu 38 : 9
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

Yeremia 4 : 23
23 ② Niliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; niliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.

Mwanzo 1 : 5
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

Isaya 45 : 7
7 Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.

Kutoka 10 : 22
22 Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu;

Zaburi 105 : 28
28 ⑩ Alituma giza, na kufanya nchi kuwa na giza, Wakayaasi maneno yake.

Kutoka 20 : 21
21 Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo.

Waraka kwa Waebrania 12 : 18
18 Maana hamkufikia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,

Mathayo 27 : 45
45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa.

Marko 15 : 33
33 Na ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hadi saa tisa.

Mithali 20 : 20
20 ⑪ Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu.

Isaya 8 : 22
22 nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.

Isaya 13 : 10
10 ③ Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

Yeremia 4 : 28
28 ⑥ Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.

Yeremia 13 : 16
16 Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.

Maombolezo 3 : 2
2 Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru.

Ezekieli 32 : 8
8 Mianga yote ya mbinguni iangazayo nitaifanya kuwa giza juu yako, nami nitatia giza katika nchi yako, asema Bwana MUNGU.

Yoeli 2 : 2
2 siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.

Yoeli 2 : 10
10 Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;

Amosi 4 : 13
13 ⑩ Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.

Amosi 5 : 18
18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwa nini kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.

Amosi 5 : 20
20 Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *