Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gershom
Kutoka 2 : 22
22 Huyo akamzalia mtoto wa kiume, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni.
Kutoka 18 : 3
3 pamoja na wanawe wawili; katika hao, jina la mmoja ni Gershomu, maana alisema, Mimi nimekuwa mgeni katika nchi za kigeni;[23]
1 Mambo ya Nyakati 23 : 16
16 Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.
Ezra 8 : 2
2 Wa uzao wa Finehasi, Gershomu; wa wana wa Ithamari, Danieli; wa wana wa Daudi, Hatushi, mwana wa Shekania;
Waamuzi 18 : 30
30 Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga; na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni makuhani katika kabila la Wadani hadi siku nchi hiyo ilipochukuliwa mateka.
Leave a Reply