Biblia inasema nini kuhusu Gereza – Mistari yote ya Biblia kuhusu Gereza

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gereza

Mwanzo 39 : 20
20 ⑤ Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani.

Mwanzo 42 : 19
19 Kama ninyi ni wa kweli, mmoja wenu na afungwe gerezani, nanyi mwende mkachukue nafaka kwa ajili ya njaa ya nyumba zenu,

Mambo ya Walawi 24 : 12
12 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa BWANA.

Hesabu 15 : 34
34 Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.

Ezra 7 : 26
26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kali, iwe ni kuuawa, au ni kuhamishwa, au kunyang’anywa mali yake, au kufungwa.

Yeremia 52 : 11
11 ⑥ Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake.

Luka 23 : 19
19 Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina iliyotokea mjini, na kwa uuaji

Matendo 4 : 3
3 Wakawakamata, wakawaweka gerezani hadi asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.

Matendo 12 : 5
5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

Matendo 5 : 18
18 wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;

Matendo 16 : 24
24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *