Biblia inasema nini kuhusu Gari – Mistari yote ya Biblia kuhusu Gari

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gari

Kutoka 14 : 7
7 tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maofisa wa kijeshi juu ya magari hayo yote.

Kutoka 14 : 9
9 ② Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi wote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata wakiwa wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni.

Kutoka 14 : 25
25 Akayakwamisha[15] magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.

Yoshua 11 : 4
4 ⑩ Nao wakatoka nje, wao na mjeshi yao yote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.

1 Samweli 13 : 5
5 ⑪ Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.

1 Wafalme 20 : 1
1 ⑩ Basi, Ben-hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.

1 Wafalme 20 : 25
25 Kisha ujihesabie jeshi, kama jeshi ulilopoteza, farasi kwa farasi na gari kwa gari; nasi tutapigana nao katika nchi tambarare, na bila shaka tutawashinda. Akaisikiliza sauti yao, akafanya kama hivyo.

2 Wafalme 6 : 14
14 Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.

2 Mambo ya Nyakati 12 : 3
3 akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.

Zaburi 20 : 7
7 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.

Zaburi 46 : 9
9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.

Yeremia 46 : 9
9 Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.

Yeremia 47 : 3
3 Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;

Yeremia 51 : 21
21 na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

Yoeli 2 : 5
5 Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita.

Nahumu 2 : 4
4 Magari ya vita yanafanya vishindo njiani, Yanasonganasongana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.

Nahumu 3 : 2
2 Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka;

Kutoka 14 : 25
25 Akayakwamisha[15] magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.

Kutoka 14 : 7
7 tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maofisa wa kijeshi juu ya magari hayo yote.

1 Wafalme 9 : 22
22 Lakini kwa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu yeyote shokoa; ila wao walikuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maafisa wake, makamanda wa magari yake na wapanda farasi wake.

1 Wafalme 22 : 33
33 Ikawa, wakuu wa magari walipoona ya kuwa siye mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate.

2 Wafalme 8 : 21
21 Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na makamanda wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao.

Yoshua 17 : 18
18 lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa sasa ni msitu, wewe utaufyeka, na kuimiliki yote hadi mwisho wake; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.

Waamuzi 1 : 19
19 BWANA alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi yenye milima; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *