Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia furaha
Warumi 12 : 12
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
Wafilipi 4 : 4
4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
Yakobo 1 : 2
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
Wagalatia 5 : 22
22 ⑮ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
Warumi 15 : 13
13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Yohana 16 : 24
24 Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
1 Petro 1 : 8
8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
Warumi 14 : 17
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Zaburi 16 : 9
9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Yohana 16 : 22
22 ⑲ Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Yakobo 1 : 2 – 4
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
1 Wathesalonike 5 : 16
16 Furahini siku zote;
1 Wathesalonike 2 : 20
20 Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu.
Mithali 17 : 22
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
2 Wakorintho 7 : 4
4 Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.
Mithali 10 : 28
28 Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali matarajio yao wasio haki yatapotea.
Luka 15 : 10
10 ⑮ Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
1 Yohana 1 : 4
4 Na haya tunayaandika, ili furaha yetu itimizwe.
Isaya 55 : 12
12 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya shambani itapiga makofi.
Zaburi 4 : 7
7 Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
Leave a Reply