Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Flint
Kumbukumbu la Torati 8 : 15
15 ⑰ aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,
Kumbukumbu la Torati 32 : 13
13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
Zaburi 114 : 8
8 Augeuzaye mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.
Isaya 50 : 7
7 ③ Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Ezekieli 3 : 9
9 ⑦ Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.
Leave a Reply