Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia fedha za mkopo
Kutoka 22 : 25
25 Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Kumbukumbu la Torati 23 : 19 โ 20
19 Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu chochote kikopeshwacho kwa riba;
20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
Mithali 19 : 17
17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
1 Yohana 3 : 17
17 โณ Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
Mambo ya Walawi 25 : 35 โ 55
35 โณ Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.
36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.
37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.
38 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.
39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimfanye akutumikie kama mtumwa;
40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hadi mwaka wa jubilii;
41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.
42 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe kama watumwa.
43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako.
44 Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi.
45 Tena wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.
46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumishi wenu kwa hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli.
47 Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni;
48 baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa;
49 au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe.
50 Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa jubilii; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo.
51 Ikiwa ingali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo.
52 Tena kama imesalia miaka michache tu hadi mwaka wa jubilii, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake.
53 Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hadi mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako.
54 Tena kwamba hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, ndipo atatoka katika mwaka wa jubilii, yeye, pamoja na watoto wake.
55 Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Mithali 22 : 7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
Warumi 13 : 8
8 โข Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Leave a Reply