Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Fedha
Ezekieli 27 : 12
12 Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa.
Mithali 17 : 3
3 ⑲ Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.
Mithali 25 : 4
4 Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
Mithali 26 : 23
23 Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
Ezekieli 22 : 22
22 Kama fedha iyeyushwavyo katika tanuri, ndivyo mtakavyoyeyushwa katikati mwake; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.
Yeremia 6 : 30
30 ⑧ Watu watawaita taka za fedha, kwa sababu BWANA amewakataa.
Zekaria 13 : 9
9 Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Mwanzo 13 : 2
2 ② Naye Abramu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.
Mwanzo 17 : 12
12 ⑯ Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
Mwanzo 20 : 16
16 Naye akamwambia Sara, Tazama! Nimempa ndugu yako fedha elfu moja, itakuwa kifunika macho kwako mbele ya wote walio pamoja nawe, nawe utakuwa na haki mbele ya watu wote.
Mwanzo 23 : 16
16 ④ Abrahamu akakubali maneno ya Efroni. Abrahamu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
Amosi 8 : 6
6 tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano.
Mathayo 10 : 9
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala pesa mishipini mwenu;
Mathayo 26 : 15
15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.[7]
Marko 14 : 11
11 Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa.
Kutoka 26 : 19
19 ③ Nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile mbao ishirini, vitako viwili chini ya ubao mmoja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya ubao mwingine kupokea zile ndimi zake mbili;
Kutoka 27 : 17
17 Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.
Kutoka 35 : 24
24 Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya BWANA; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yoyote ya huo utumishi, akauleta.
Leave a Reply