Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Farao
Mwanzo 12 : 20
20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.
Zaburi 105 : 14
14 Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 18
18 Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.
1 Wafalme 11 : 22
22 Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu.
1 Wafalme 3 : 1
1 Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya BWANA, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.
1 Wafalme 9 : 16
16 Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani.
2 Wafalme 18 : 21
21 ⑫ Sasa tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo mtu akiitegemea, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
2 Wafalme 23 : 35
35 Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao Neko.
2 Wafalme 24 : 7
7 Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang’anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
2 Mambo ya Nyakati 35 : 24
24 Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakamlilia Yosia.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 4
4 Mfalme wa Misri akamtawaza Eliakimu nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Neko akamtwaa Yehoahazi nduguye, akamchukua mpaka Misri.
Yeremia 46 : 2
2 ⑩ Kuhusu Misri; habari za jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri, lililokuwa karibu na mto Frati katika Karkemishi, ambalo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilipiga katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda.
Yeremia 47 : 1
1 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.
Leave a Reply