Biblia inasema nini kuhusu familia – Mistari yote ya Biblia kuhusu familia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia familia

Waefeso 6 : 1 – 4
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 ① Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

1 Timotheo 3 : 5
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)

1 Timotheo 3 : 4
4 ⑤ mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

Mwanzo 50 : 17 – 21
17 ⑯ Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwasamehe ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utusamehe kosa la watumishi wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.
18 ⑰ Ndugu zake wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumishi wako.
19 ⑱ Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu?
20 ⑲ Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
21 ⑳ Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *