Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ethanimu
Mambo ya Walawi 23 : 25
25 Msifanye kazi yoyote ya utumishi; nanyi mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto.
Mambo ya Walawi 23 : 32
32 Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtajinyima; siku ya tisa ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hadi jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Mambo ya Walawi 23 : 43
43 ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa niliwafanya wana wa Israeli kukaa katika vibanda, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
Mambo ya Walawi 25 : 9
9 ⑥ Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
1 Wafalme 8 : 2
2 Watu wote wa Israeli wakakutana mbele ya mfalme Sulemani wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu,[16] ndio mwezi wa saba.
Ezra 3 : 1
1 Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu.
Ezra 3 : 6
6 Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la BWANA ulikuwa haujawekwa bado.
Leave a Reply