Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Eshtaol
Yoshua 15 : 33
33 Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, Sora, Ashna,
Yoshua 19 : 41
41 ⑲ Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, Eshtaoli, Irishemeshi;
Waamuzi 18 : 2
2 Basi wana wa Dani wakatuma watu watano kutoka kwa koo zao zote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuikagua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hadi nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko.
Waamuzi 18 : 8
8 Kisha wakawarudia ndugu zao huko Sora na Eshtaoli; ndugu zao wakawauliza; Haya, mna habari gani?
Waamuzi 18 : 11
11 Basi wakatoka hapo watu mia sita waliovaa silaha za vita, wa jamaa ya Wadani, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli.
Waamuzi 13 : 25
25 Roho ya BWANA ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.
Waamuzi 16 : 31
31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakateremka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Leave a Reply