Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ensign
Zaburi 74 : 4
4 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako; Wameweka bendera zao ziwe alama.
Isaya 5 : 26
26 Naye atawatolea ishara mataifa toka mbali, Naye atawapigia miruzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.
Isaya 11 : 10
10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa makabila ya watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.
Isaya 11 : 12
12 Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.
Isaya 18 : 3
3 Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.
Isaya 30 : 17
17 Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Isaya 31 : 9
9 Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema BWANA, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuri yake katika Yerusalemu.
Leave a Reply