Biblia inasema nini kuhusu Elkana – Mistari yote ya Biblia kuhusu Elkana

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Elkana

Kutoka 6 : 24
24 Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 23
23 na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri;

1 Samweli 1 : 1
1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu

1 Samweli 1 : 4
4 Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, wanaume kwa wanawake, sehemu zao;

1 Samweli 1 : 8
8 Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwa nini huli? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi?

1 Samweli 1 : 19
19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.

1 Samweli 1 : 21
21 Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake.

1 Samweli 1 : 23
23 Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hadi utakapomwachisha kunyonya; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hadi akamwachisha kunyonya.

1 Samweli 2 : 11
11 ② Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA mbele yake Eli, kuhani.

1 Samweli 2 : 20
20 Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, wachukue mahali pa yule aliyemtoa kwa BWANA. Kisha wakarudi nyumbani kwao.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 27
27 na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 34
34 mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

1 Mambo ya Nyakati 6 : 25
25 Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 36
36 mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;

1 Mambo ya Nyakati 6 : 26
26 Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu;

1 Mambo ya Nyakati 6 : 35
35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;

1 Mambo ya Nyakati 9 : 16
16 na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.

1 Mambo ya Nyakati 12 : 6
6 Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora;

1 Mambo ya Nyakati 15 : 23
23 Na Berekia na Elkana walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *