Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Elifazi
Mwanzo 36 : 4
4 Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli.
Mwanzo 36 : 16
16 jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 35
35 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.
Ayubu 2 : 11
11 Basi ikawa hao marafiki watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumfariji Ayubu na kumtuliza moyo.
Ayubu 42 : 9
9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile BWANA alivyowaamuru; naye BWANA akamridhia Ayubu.
Leave a Reply