Biblia inasema nini kuhusu Eliabu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Eliabu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Eliabu

Hesabu 26 : 9
9 Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA;

Hesabu 16 : 1
1 Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;

Hesabu 16 : 12
12 Kisha Musa akatuma ujumbe wa kuwaita Dathani na Abiramu wana wa Eliabu; nao wakasema, “Hatuji sisi”;

Kumbukumbu la Torati 11 : 6
6 ⑰ na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;

Hesabu 1 : 9
9 Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni.

Hesabu 2 : 7
7 ① na kabila la Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;

Hesabu 7 : 24
24 Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni;

Hesabu 7 : 29
29 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Eliabu mwana wa Heloni.

Hesabu 10 : 16
16 Na juu ya jeshi la kabila la wana wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 27
27 na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana.

1 Samweli 1 : 1
1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu

1 Mambo ya Nyakati 6 : 34
34 mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

1 Samweli 16 : 6
6 Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi[19] wa BWANA yupo hapa mbele zake.

1 Samweli 17 : 13
13 ① Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya, mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu Shama.

1 Samweli 17 : 28
28 ⑥ Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 13
13 ⑫ na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

1 Mambo ya Nyakati 27 : 18
18 wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;

1 Mambo ya Nyakati 12 : 9
9 Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *