Biblia inasema nini kuhusu Elamu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Elamu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Elamu

Mwanzo 14 : 1
1 ⑮ Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu,

Mwanzo 14 : 9
9 wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano.

Danieli 8 : 2
2 Nami niliona katika maono; nilipokuwa natazama na nikajionea mwenyewe nikiwa huko Susa, Mji mkuu wa mkoa wa Elamu; nikaona katika maono, nami nilikuwa karibu na mto Ulai.

Isaya 11 : 11
11 Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.

Isaya 21 : 2
2 ⑰ Nimeoneshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.

Isaya 22 : 6
6 Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao.

Yeremia 25 : 25
25 na wafalme wote wa Zimri, na wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi;

Yeremia 49 : 39
39 Lakini itakuwa, katika siku za mwisho, nitawarudisha wafungwa wa Elamu, asema BWANA.

Ezekieli 32 : 24
24 ② Elamu yuko huko, na watu wake umati wote, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka wakiwa hawajatahiriwa hadi pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.

1 Mambo ya Nyakati 26 : 3
3 Elamu wa tano, Yohana wa sita, Elioenai wa saba.

1 Mambo ya Nyakati 8 : 24
24 na Hanania, na Elamu, na Anthothiya;

Ezra 2 : 31
31 Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

Nehemia 7 : 34
34 Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

Ezra 2 : 7
7 Wazawa wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

Ezra 8 : 7
7 Na wa wana wa Elamu, Yeshaya, mwana wa Athalia; na pamoja naye wanaume sabini.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *