Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ekaristi
Mathayo 26 : 30
30 ⑥ Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda katika mlima wa Mizeituni.
Marko 14 : 24
24 ③ Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.
Luka 22 : 20
20 ⑬ Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Yohana 13 : 4
4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
Luka 13 : 26
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
Matendo 2 : 42
42 ⑳ Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Matendo 2 : 47
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Matendo 20 : 7
7 ⑪ Siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubia, maana aliazimia kusafiri siku iliyofuata, naye akafululiza maneno yake hadi usiku wa manane.
1 Wakorintho 10 : 17
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
1 Wakorintho 10 : 22
22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
1 Wakorintho 11 : 34
34 mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.
Leave a Reply