Biblia inasema nini kuhusu Efroni – Mistari yote ya Biblia kuhusu Efroni

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Efroni

Mwanzo 23 : 17
17 ⑤ Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango lililokuwemo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa

Mwanzo 25 : 9
9 ⑮ Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.

Mwanzo 49 : 30
30 ⑤ katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

Mwanzo 50 : 13
13 ⑭ kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

Yoshua 15 : 9
9 kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hadi kufika chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hadi kufika Baala (ndio Kiriath-yearimu);

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *