Biblia inasema nini kuhusu Efodi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Efodi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Efodi

Kutoka 28 : 14
14 na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo.

Kutoka 28 : 35
35 Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikika hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya BWANA na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.

Kutoka 25 : 7
7 na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.

Kutoka 39 : 26
26 njuga na komamanga, njuga na komamanga katika pindo za joho kuizunguka pande zote, ili kutumika kwa hiyo; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Kutoka 28 : 29
29 Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya BWANA daima.

Kutoka 39 : 5
5 ⑦ Na huo mshipi wa kazi ya werevu, uliokuwa juu yake ili kuifunga mahali pake; ulikuwa wa kitu kimoja, na wa kazi moja na naivera ya dhahabu, na rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.

1 Samweli 23 : 9
9 ⑩ Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera.

1 Samweli 23 : 12
12 Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? BWANA akasema, Watakutia.

1 Samweli 30 : 8
8 Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.

1 Samweli 22 : 18
18 ① Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, uwaangukie hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani.

1 Samweli 2 : 18
18 ⑤ Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana aliyevaa naivera ya kitani.

2 Samweli 6 : 14
14 ⑲ Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

Kutoka 28 : 40
40 Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.

Kutoka 29 : 8
8 Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu.

Kutoka 39 : 27
27 ⑰ Nao wakafanya hizo kanzu za nguo ya kitani nzuri ya kufumwa, kwa Haruni, na kwa wanawe

Kutoka 40 : 14
14 Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;

Mambo ya Walawi 8 : 13
13 Kisha Musa akawaleta wana wa Haruni, na kuwavika kanzu, na kuwafunga mishipi, na kuwavika vilemba; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Mambo ya Walawi 10 : 5
5 Basi wakaja karibu, na kuwachukua, wakiwa wamevaa nguo zao, wakawachukua nje ya kambi; kama Musa alivyosema.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *