Biblia inasema nini kuhusu Ebal – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ebal

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ebal

1 Mambo ya Nyakati 1 : 22
22 na Obali, na Abimaeli, na Sheba;

Mwanzo 36 : 23
23 Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu.

1 Mambo ya Nyakati 1 : 40
40 Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.

Kumbukumbu la Torati 11 : 29
29 Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.

Kumbukumbu la Torati 27 : 13
13 na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.

Yoshua 8 : 33
33 ② Na Israeli wote pamoja na wazee, viongozi wao na waamuzi wao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyoamuru hapo awali, ili wawabariki watu wa Israeli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *