Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dor
Yoshua 11 : 2
2 ⑦ na hao wafalme waliokuwa upande wa kaskazini, katika nchi ya vilima, na katika Araba upande wa kusini wa Kinerethi, na katika Shefela, na katika nchi tambarare za Dori upande wa magharibi,
Yoshua 12 : 23
23 mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja;
1 Wafalme 4 : 11
11 Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake.
Yoshua 17 : 11
11 Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, na pia theluthi ya Nafathi.
Waamuzi 1 : 27
27 Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Beth-sheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo.
Leave a Reply