Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Doeg
1 Samweli 21 : 7
7 Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za BWANA jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli.
1 Samweli 22 : 9
9 Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu.
1 Samweli 22 : 22
22 Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nilijua hakika ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo.
Zaburi 52 : 1
1 ⑧ Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.
1 Samweli 22 : 19
19 ② Kisha akaupiga Nobu, mji wa makuhani, kwa makali ya upanga, wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, na ng’ombe, na punda, na kondoo.
Leave a Reply