Biblia inasema nini kuhusu Dodo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Dodo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dodo

Waamuzi 10 : 1
1 ⑳ Baada yake Abimeleki, akainuka Tola mwana wa Pua, mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, kuwaokoa Israeli; naye alikuwa akikaa Shamiri, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu.

2 Samweli 23 : 9
9 Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;

1 Mambo ya Nyakati 11 : 12
12 Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.

1 Mambo ya Nyakati 27 : 4
4 Na juu ya zamu ya mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mwahohi, na zamu yake; na Miklothi alikuwa afisa mkuu; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.

2 Samweli 23 : 24
24 Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu;

1 Mambo ya Nyakati 11 : 26
26 ⑯ Tena hawa ndio mashujaa wa majeshi ya askari; Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *