Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Daudi
1 Mambo ya Nyakati 12 : 23 – 40
23 Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumpa ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la BWANA.
24 Wana wa Yuda, waliochukua ngao na mkuki, walikuwa elfu sita na mia nane, wenye silaha za vita.
25 Wa wana wa Simeoni, wanaume mashujaa wa vita, elfu saba na mia moja.
26 Wa wana wa Lawi, elfu nne na mia sita.
27 Na Yehoyada alikuwa kichwa cha ukoo wa Haruni, na pamoja naye walikuwa watu elfu tatu na mia saba;
28 tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, makamanda ishirini na wawili.
29 Na wa wana wa Benyamini nduguze Sauli, elfu tatu; kwani hata sasa walio wengi wao walikuwa wameuhifadhi uaminifu wao kwa nyumba ya Sauli.
30 Na wa wana wa Efraimu, elfu ishirini na mia nane, wanaume mashujaa, watu wenye sifa katika koo za baba zao.
31 Na wa nusu kabila la Manase, elfu kumi na nane, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme.
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
33 Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, elfu hamsini; askari stadi waliolenga tu kumsaidia Daudi.
34 Na wa Naftali, makamanda elfu moja, na pamoja nao watu wenye ngao na mkuki elfu thelathini na saba.
35 Na wa Wadani, watu hodari wa kupanga vita, elfu ishirini na nane na mia sita.
36 Na wa Asheri, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, elfu arubaini.
37 Tena, ng’ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila la Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, elfu mia moja na ishirini.
38 Hao wote, watu wa vita, askari stadi, wakaja Hebroni wakiwa na nia moja ya kumtawaza Daudi awe mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja kwamba wamtawaze Daudi.
39 Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.
40 Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng’ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng’ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli.
1 Mambo ya Nyakati 18 : 14
14 Basi Daudi akawatawala Waisraeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.
2 Samweli 5 : 5
5 Huko Hebroni alitawala miaka saba na miezi sita; na katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya Israeli wote na Yuda.
Zaburi 26 : 1 – 12
1 Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
2 Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu.
3 Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.
4 Sikai pamoja na watu waovu, Wala sitaingia kuwa pamoja na wanafiki.
5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu.
6 Nitanawa mikono yangu bila ya kuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA
7 Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.
8 BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako.
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji.
10 Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kulia umejaa rushwa.
11 Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili.
12 Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika kusanyiko kuu nitamhimidi BWANA.
Zaburi 35 : 1 – 28
1 Ee BWANA, uwapinge hao wanaonipinga, Upigane nao wanaopigana nami.
2 Uishike ngao na kikingio, Uinuke unisaidie.
3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
4 Waaibike na kufedheheka, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.
5 Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa BWANA akiwaangusha chini.
6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia.
7 Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.
8 ⑮ Uharibifu na umpate kwa ghafla, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
9 ⑯ Na nafsi yangu itamfurahia BWANA, Na kuushangilia wokovu wake.
10 ⑰ Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
11 Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua.
12 Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.
13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nilijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
14 Nilisikitika kana kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Niliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
15 Lakini nikijikwaa wanafurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wakanipapura bila kukoma.
16 Bila heshima walinidhihaki kupindukia, Wakanisagia meno yao.
17 BWANA, utatazama hadi lini? Uiokoe nafsi yangu kutoka kwa maangamizi yao, Na maisha yangu kutoka kwa wanasimba.
18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.
19 ⑱ Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e.
20 Maana hawasemi maneno ya amani, Ila juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.
21 Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.
22 ⑲ Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami.
23 Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
24 ⑳ Unihukumu kwa haki yako, Ee BWANA, Mungu wangu, Na usiwaache wanisimange.
25 Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza.
26 Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.
27 Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
28 Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
Leave a Reply