Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dario
Danieli 5 : 31
31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.
Danieli 9 : 1
1 Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;
Hagai 1 : 1
1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,
Hagai 1 : 15
15 katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa mfalme Dario.
Zekaria 1 : 1
1 Katika mwezi wa nane, mwaka wa pili wa Dario, neno la BWANA lilimjia Zekaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, nabii, kusema,
Nehemia 12 : 22
22 Walawi siku za Eliashibu, na Yoyada, na Yohana, na Yadua, wameorodheshwa wakuu wa mbari za mababa; tena na makuhani; hata siku za kumiliki kwake Dario, Mwajemi.
Leave a Reply