Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dan
Mwanzo 30 : 6
6 Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Mwanzo 35 : 25
25 Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.
Mwanzo 46 : 23
23 Na wana wa Dani; Hushimu.
Hesabu 26 : 43
43 Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.
Mwanzo 49 : 17
17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Na apandaye akaanguka chali.
Hesabu 1 : 39
39 wale waliohesabiwa katika kabila la Dani, walikuwa watu elfu sitini na mbili na mia saba (62,700).
Hesabu 26 : 43
43 Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.
Yoshua 19 : 47
47 Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.
Ezekieli 48 : 1
1 Basi, haya ndiyo majina ya makabila hayo; toka mwisho wa pande za kaskazini, karibu na njia ya Hethloni, hadi maingilio ya Hamathi, hadi Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, yaani, upande wa kaskazini karibu na Hamathi, watakuwa na upande wa mashariki, na upande wa magharibi; Dani fungu moja.
Hesabu 2 : 25
25 ⑩ Upande wa kaskazini kutakuwa na bendera ya kambi ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai.
Hesabu 2 : 31
31 ⑫ Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera[2] yao.
Hesabu 10 : 25
25 ⑪ Kisha beramu ya kambi ya wana wa Dani, ambayo ilikuwa ni nyuma ya makambi yote, ikasafiri, kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
Kumbukumbu la Torati 33 : 22
22 Na Dani akamnena, Dani ni mwanasimba, Arukaye kutoka Bashani.
Waamuzi 1 : 35
35 ① lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.
Leave a Reply