Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia chumvi
Mathayo 5 : 13
13 ③ Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza ladha yake, ladha hiyo itarudishwa vipi? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Wakolosai 4 : 6
6 ⑥ Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Mathayo 5 : 13 – 16
13 ③ Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza ladha yake, ladha hiyo itarudishwa vipi? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 ④ Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji ukiwa juu ya mlima hauwezi kusitirika.
15 ⑤ Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 ⑥ Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Marko 9 : 50
50 ② Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
Luka 14 : 34 – 35
34 ⑩ Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?
35 Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.
Marko 9 : 49
49 ① Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.
Hesabu 18 : 19
19 Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.
Marko 9 : 49 – 50
49 ① Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.
50 ② Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
2 Wafalme 2 : 20 – 22
20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea.
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
Mwanzo 19 : 26
26 ⑳ Lakini mkewe Lutu, akiwa nyuma ya mumewe, aliangalia nyuma akawa nguzo ya chumvi.
Luka 14 : 34
34 ⑩ Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?
Mambo ya Walawi 2 : 13
13 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
2 Wafalme 2 : 21
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
Ezekieli 43 : 24
24 ⑫ Nawe utawaleta karibu mbele za BWANA, na makuhani watamwaga chumvi juu yao, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa BWANA.
Ayubu 6 : 6
6 Je! Kitu kisicho na ladha chaweza kulika bila chumvi? Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?
2 Wafalme 14 : 7
7 ⑪ Akawaua Waedomi katika Bonde la Chumvi watu elfu kumi; akautwaa Sela vitani, akauita jina lake Yoktheeli hata leo.
2 Mambo ya Nyakati 13 : 5
5 ⑧ je! Haikuwapasa kujua ya kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?
Ezra 6 : 9
9 Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng’ombe wachanga, na kondoo dume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;
2 Wafalme 2 : 20
20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea.
Sefania 2 : 9
9 Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Leave a Reply