Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia chuki
1 Yohana 4 : 20
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
1 Yohana 3 : 15
15 ⑱ Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukaao ndani yake.
Mithali 10 : 12
12 ⑮ Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
Mithali 6 : 16 – 19
16 Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 ⑤ Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 ⑥ Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 ⑦ Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Warumi 1 : 26 – 27
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
Waefeso 4 : 29
29 ⑮ Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Mambo ya Walawi 19 : 17
17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, au ulipizwe uovu kwa ajili yake
1 Wakorintho 13 : 4 – 7
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Mithali 15 : 1
1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Yohana 13 : 34 – 35
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Mathayo 6 : 24
24 ③ Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Mithali 8 : 13
13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mathayo 10 : 22
22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Zaburi 101 : 3
3 Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.
Zaburi 97 : 10
10 ⑯ Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
Warumi 6 : 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Malaki 1 : 3
3 bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.
Mathayo 10 : 34
34 ⑧ Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
Zaburi 119 : 163
163 Nimeuchukia uongo, umenikirihi, Sheria yako nimeipenda.
Leave a Reply