Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Chui
Wimbo ulio Bora 4 : 8
8 ① Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui.
Yeremia 5 : 6
6 ⑯ Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Yeremia 13 : 23
23 Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.
Hosea 13 : 7
7 Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani;
Habakuki 1 : 8
8 Farasi wao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwamwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.
Danieli 7 : 6
6 ⑧ Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
Isaya 11 : 6
6 Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng’ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Leave a Reply