Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bwawa
1 Wafalme 22 : 38
38 Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la BWANA alilolinena.
2 Wafalme 18 : 17
17 ⑧ Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na kamanda wake,[11] toka Lakishi, kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika, wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
Isaya 36 : 2
2 Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri[8] toka Lakishi pamoja na jeshi kubwa kwenda hadi Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Naye akasimama karibu na mfereji wa bwawa la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
Isaya 22 : 9
9 Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini.
Nehemia 3 : 15
15 ⑩ Na lango la chemchemi akalijenga Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa Mispa akalitengeneza lango la Chemchemi akalijenga na kulifunika, akasimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.
Yohana 9 : 7
7 akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona.
Yohana 9 : 11
11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.
Wimbo ulio Bora 7 : 4
4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski;
Leave a Reply