Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bwana Harusi
Isaya 61 : 10
10 Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Kumbukumbu la Torati 24 : 5
5 ④ Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.
Waamuzi 14 : 11
11 Basi ikawa hapo watu walipomwona, wakamletea wenziwe thelathini, wawe pamoja naye.
Mathayo 9 : 15
15 ⑰ Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
Marko 2 : 20
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku ile.
Luka 5 : 35
35 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile.
Mathayo 25 : 13
13 ⑲ Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Wimbo ulio Bora 4 : 16
16 ⑥ Amka, kaskazi; nawe uje, kusi; Vumeni juu ya bustani yangu, Manukato ya bustani yatokee. Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, Akayale matunda yake mazuri.
Ezekieli 16 : 14
14 Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU.
Leave a Reply