Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Busu
Mwanzo 27 : 27
27 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.
Mwanzo 31 : 55
55 Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.
Mwanzo 33 : 4
4 Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.
Mwanzo 48 : 10
10 Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona vizuri. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia.
Mwanzo 50 : 1
1 ⑦ Yusufu akamwangukia babaye usoni, akamlilila, akambusu.
Kutoka 18 : 7
7 Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.
Ruthu 1 : 14
14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye.
2 Samweli 14 : 33
33 ③ Basi Yoabu akamwendea mfalme, akamwambia hayo, naye alipomwita Absalomu, yeye akaja kwa mfalme, akainama kifudifudi hadi chini mbele ya mfalme; naye mfalme akambusu Absalomu.
2 Samweli 19 : 39
39 ⑦ Basi watu wote wakavuka Yordani, naye mfalme akavuka; kisha mfalme akambusu Barzilai, akambariki; naye akarudi nyumbani kwake.
Luka 15 : 20
20 Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
Matendo 20 : 37
37 Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusubusu,
Luka 7 : 38
38 ⑫ Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
Mithali 27 : 6
6 Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu.
2 Samweli 20 : 10
10 Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
Mathayo 26 : 48
48 Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.
Luka 22 : 48
48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
Warumi 16 : 16
16 ⑧ Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.
2 Wakorintho 13 : 12
12 ⑥ Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wanawasalimu.
1 Wathesalonike 5 : 26
26 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu.
1 Petro 5 : 14
14 Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina.
Leave a Reply