Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Busara
Ayubu 34 : 4
4 Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu; Na tujue wenyewe yaliyo mema.
Zaburi 39 : 1
1 ⑧ Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.
Zaburi 112 : 5
5 ⑱ Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.
Mithali 6 : 2
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Mithali 8 : 12
12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara.
Mithali 11 : 13
13 Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
Mithali 11 : 15
15 Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yuko salama.
Mithali 11 : 29
29 Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.
Mithali 12 : 8
8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.
Mithali 12 : 16
16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Mithali 12 : 23
23 Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
Mithali 13 : 16
16 ⑰ Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu.
Mithali 14 : 8
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
Mithali 14 : 16
16 Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.
Mithali 14 : 18
18 Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa.
Mithali 15 : 5
5 Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara.
Mithali 15 : 22
22 Pasipo ushauri mipango vuhunjika; Bali kwa wingi wa washauri huthibitika.
Mithali 16 : 21
21 Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu.
Mithali 17 : 2
2 Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
Mithali 17 : 18
18 Asiye na hekima hupeana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.
Mithali 18 : 16
16 Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu.
Mithali 19 : 2
2 Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
Mithali 20 : 5
5 Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.
Mithali 20 : 16
16 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.
Mithali 20 : 18
18 Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.
Mithali 21 : 5
5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
Mithali 21 : 20
20 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
Leave a Reply