Biblia inasema nini kuhusu Bosra – Mistari yote ya Biblia kuhusu Bosra

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bosra

Mwanzo 36 : 33
33 Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.

Mika 2 : 12
12 Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia; Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli; Nitawaweka pamoja kama kondoo katika zizi; Kama kundi la kondoo katika malisho yao; Watafanya mvumo kwa wingi wa watu;

Isaya 34 : 6
6 Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.

Isaya 63 : 1
1 ④ Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.

Yeremia 49 : 13
13 Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.

Yeremia 49 : 22
22 Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.

Amosi 1 : 12
12 lakini nitatuma moto juu ya Temani, nao utayateketeza majumba ya Bosra.

Yeremia 48 : 24
24 na juu ya Keriothi, na juu ya Bozra, na juu ya miji yote ya nchi ya Moabu, iliyo mbali na iliyo karibu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *