Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bonde
1 Wafalme 7 : 50
50 na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu.
1 Mambo ya Nyakati 28 : 17
17 na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa matasa ya dhahabu, kwa uzani kwa kila tasa; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa;
2 Mambo ya Nyakati 4 : 8
8 ⑰ Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu.
2 Mambo ya Nyakati 4 : 22
22 na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.
Ezra 1 : 10
10 mabakuli ya dhahabu thelathini, mabakuli ya fedha ya namna ya pili mia nne na kumi,[3] na vyombo vingine elfu moja.
Ezra 8 : 27
27 na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu moja; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong’aa, thamani yake sawa na dhahabu.
Kutoka 27 : 3
3 ⑮ Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
Kutoka 38 : 3
3 Kisha akafanya vyombo vyote vya madhabahu, yaani sufuria zake, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote akavifanya vya shaba.
Leave a Reply