Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Birika
Kutoka 30 : 20
20 hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea BWANA sadaka ya moto;
Kutoka 40 : 7
7 Kisha utaliweka birika kati ya hema ya kukutania na hiyo madhabahu, nawe utatia maji ndani yake.
Kutoka 30 : 28
28 na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja na vyombo vyake vyote, na birika, na kitako chake.
Kutoka 40 : 11
11 Kisha utalitia mafuta birika na kitako chake, na kuliweka liwe takatifu.
Mambo ya Walawi 8 : 11
11 Kisha akanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kuitia mafuta madhabahu na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake, ili kuvitakasa.
Kutoka 40 : 32
32 ③ hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.
1 Wafalme 7 : 26
26 ⑬ Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi[14] elfu mbili.
1 Wafalme 7 : 30
30 Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni.
1 Wafalme 7 : 39
39 Akaviweka vile vitako, vitano upande wa kulia wa nyumba, na vitano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kulia wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini.
2 Mambo ya Nyakati 4 : 14
14 Akatengeneza vitako, akatengeneza na mabeseni juu ya vitako;
2 Wafalme 16 : 17
17 ⑧ Mfalme Ahazi akakata papi za vitako, akaliondoa lile birika juu yake; akaiteremsha ile bahari itoke juu ya ng’ombe za shaba zilizokuwa chini yake, akaiweka juu ya sakafu ya mawe.
2 Wafalme 25 : 13
13 ⑮ Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na vitako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
2 Wafalme 25 : 16
16 Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na vile vitako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
Yeremia 52 : 17
17 ⑩ Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya BWANA, na vikalio vya mazulia ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya BWANA, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Yeremia 52 : 20
20 Nguzo mbili, beseni, na ng’ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya vikalio vyake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana.
Ufunuo 4 : 6
6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
Ufunuo 15 : 2
2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi vya Mungu.
Kutoka 38 : 8
8 Kisha akafanya hilo birika la shaba, na kitako chake cha shaba; shaba hiyo ilikuwa ni ya vioo vya wanawake wenye kutumika, waliokuwa wakitumika mlangoni mwa hema ya kukutania.
1 Wafalme 7 : 23
23 ⑩ Tena akatengeneza bahari[11] ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.
Leave a Reply