Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia binti Sayuni
Zekaria 9 : 9
9 ⑫ Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Isaya 3 : 16 – 26
16 BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao.
18 Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
19 na pete za masikio, na vikuku, na mataji yao;
20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;
21 na pete, na azama,
22 na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko;
23 na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.
24 Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
25 Watu wako wanaume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.
26 ⑦ Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.
Maombolezo 1 : 1 – 22
1 Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!
2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake.
3 Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya mataifa, Haoni raha yoyote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake.
4 Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.
5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.
7 Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamanio yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
8 Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.
9 Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.
10 Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.
11 Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
12 Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.
13 Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu, Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu, Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.
14 Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;
15 Bwana amenitia mikononi mwao, Ambao siwezi kupingamana nao. Bwana amewafanya mashujaa wangu wote Kuwa si kitu kati yangu; Ameita mkutano mkuu kinyume changu Ili kuwaponda vijana wangu; Bwana amemkanyaga kama shinikizoni Huyo bikira binti Yuda.
16 Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; BWANA ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
18 BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
19 Niliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao.
20 Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.
21 Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.
22 Huo uovu wao wote Na uje mbele zako wewe; Ukawatende wao kama ulivyonitenda mimi Kwa dhambi zangu zote; Kwa maana mauguzi yangu ni mengi sana, Na moyo wangu umezimia.
Zekaria 9 : 9 – 10
9 ⑫ Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
10 ⑬ Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Ezekieli 16 : 8 – 13
8 Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
9 Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nilikuosha kabisa damu yako, na kukupaka mafuta;
10 nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri.
11 Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.
12 Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.
13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.
Ufunuo 12 : 2
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, akiwa na uchungu na kuumwa katika kuzaa.
Zekaria 2 : 10
10 Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema BWANA.
1 Yohana 4 : 18
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
Matendo 10 : 34
34 ⑥ Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
Mathayo 21 : 5
5 ⑦ Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda.
Yakobo 1 : 20
20 kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
Yeremia 6 : 15 – 19
15 Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajia wataangushwa chini, asema BWANA.
16 BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
17 Nami niliweka walinzi juu yenu, wakisema, Isikilizeni sauti ya tarumbeta; lakini walisema, Hatutaki kusikiliza.
18 Kwa sababu hiyo sikilizeni, enyi mataifa, mkajue, Ee kusanyiko, ni jambo gani litokealo kati yao.
19 Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.
Ezekieli 22 : 12
12 ② Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.
Ezekieli 16 : 20 – 23
20 Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,
21 hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao?
22 Na katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, bila mavazi, ukawa ukigaagaa katika damu yako.
23 Tena, imekuwa baada ya uovu wako wote, (ole wako! ole wako! Asema Bwana MUNGU,)
Yohana 4 : 24
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Mathayo 5 : 48
48 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Yeremia 3 : 3
3 ⑫ Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika.
Luka 1 : 41 – 47
41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijie mimi?
44 Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
45 Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
46 Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
Zaburi 119 : 1 – 176
1 Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.
2 Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.
3 Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake.
4 Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana.
5 Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.
6 Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.
7 Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako.
8 Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa.
9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
12 Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.
13 Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako.
14 Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi.
15 Nitayatafakari maagizo yako, Na kuziangalia njia zako.
16 Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.
17 Umtendee mtumishi wako ukarimu, Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.
18 Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.
19 Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako.
20 Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu zako kila wakati.
21 Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.
22 Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.
23 Wakuu nao waliketi wakaninena, Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.
24 Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.
25 Nafsi yangu imegandamia mavumbini, Unihuishe sawasawa na neno lako.
26 Nilizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako.
27 Unifahamishe njia ya maagizo yako, Nami nitayatafakari maajabu yako.
28 Nafsi yangu imeyeyuka kwa huzuni, Unitie nguvu sawasawa na neno lako.
29 Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako.
30 Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu.
31 Nimeambatana na shuhuda zako, Ee BWANA, usiniaibishe.
32 Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.
33 Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hadi mwisho.
34 Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.
35 Uniendeshe katika mapito ya amri zako, Kwa maana nimependezwa nayo.
36 Unielekeze moyo wangu katika shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa.
37 Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
38 Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Iliyo ya wanaokucha.
39 Uniondolee laumu niiogopayo, Maana hukumu zako ni njema.
40 Tazama, nimeyatamani mausia yako, Unihuishe kwa haki yako.
41 Ee BWANA, fadhili zako zinifikie na mimi, Naam, wokovu wako kulingana na ahadi yako.
42 Nami nitamjibu neno anilaumuye, Kwa maana nilitumainia neno lako.
43 Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako.
44 Nami nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele.
45 Nami nitakwenda kwa uhuru, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
46 ① Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu.
47 Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda.
48 Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.
49 Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako, Ambalo kwalo umenipa tumaini.
50 ② Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, Ya kwamba ahadi yako imenipa moyo.
51 ③ Wenye kiburi wamenidharau mno, Lakini sikiuki sheria zako.
52 Ninapozikumbuka hukumu zako za tangu kale, Ee BWANA, ninafarijika.
53 ④ Ghadhabu kuu imenishika kwa sababu ya wasio haki, Waiachao sheria yako.
54 Amri zako zimekuwa nyimbo zangu, Katika nyumba yangu ya ugenini.
55 ⑤ Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee BWANA, nikaitii sheria yako.
56 Hayo ndiyo niliyokuwa nayo, Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
57 ⑥ BWANA ndiye aliye fungu langu, Ninaahidi kuyatii maneno yake.
58 Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote, Unifadhili kulingana na ahadi yako.
59 ⑦ Ninapozitafakari njia zako, Naielekeza miguu yangu kwa shuhuda zako.
60 Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.
61 Japo kamba za wasio haki zimenifunga, Siisahau sheria yako.
62 ⑧ Usiku wa manane nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
63 Mimi ni mwenzi wa watu wote wakuchao, Na wale wayatiio mausia yako.
64 ⑩ BWANA, dunia imejaa fadhili zako, Unifundishe amri zako.
65 Umemtendea mtumishi wako mema, Ee BWANA, sawasawa na neno lako.
66 Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako.
67 ⑪ Kabla sijateswa mimi nilipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako.
68 ⑫ Wewe U mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako.
69 ⑬ Wenye kiburi wamenizulia uongo, Lakini kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako.
70 ⑭ Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Lakini mimi nimeifurahia sheria yako.
71 ⑮ Ilikuwa vema kwangu kuwa niliteswa, Nipate kujifunza amri zako.
72 Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
73 ⑯ Mikono yako iliniumba na kunidhibiti, Unifahamishe nikajifunze amri zako.
74 ⑰ Wakuchao na wanione na kufurahi, Kwa sababu nimelitumainia neno lako.
75 ⑱ Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.
76 Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu, Kulingana na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77 Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.
78 ⑲ Wenye kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo, Mimi nitayatafakari mausia yako.
79 Wakuchao na wanirudie, Nao watazijua shuhuda zako.
80 ⑳ Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, Nisije mimi nikaaibika.
81 Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelitumainia neno lako.
82 Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako, Nikisema, Lini utakaponifariji?
83 Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi, Sikuzisahau amri zako.
84 Siku za mtumishi wako ni ngapi, Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia?
85 Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria yako.
86 Amri zako zote ni za kudumu, Ninateswa bila sababu, nisaidie!
87 Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako.
88 Uniponye kwa fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.
89 Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele.
90 Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi, Umeiweka nchi, nayo imethibitika.
91 Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako.
92 Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika mateso yangu.
93 Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha.
94 Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako.
95 Wasio haki wameniotea ili kunipoteza, Nitazitafakari shuhuda zako.
96 Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali amri yako haina kikomo.
97 Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.
98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote.
99 Ninazo akili kuliko waalimu wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
100 Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
101 Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako.
102 Sikuziacha hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha.
103 Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu.
104 Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
106 Nimeapa nami nikathibitisha, Kuzishika hukumu zako za haki.
107 Nimeteswa mno; Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako.
108 Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu, Na kunifundisha hukumu zako.
109 Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima, Lakini sheria yako sikuisahau.
110 Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sitoki katika njia ya mausia yako.
111 Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.
112 Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, Daima, naam, hata milele.
113 Watu wa kusitasita nawachukia, Lakini sheria yako naipenda.
114 Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea.
115 Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu.
116 Unitegemeze kulingana na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu.
117 Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima.
118 Umewakataa wote wazikosao amri zako, Kwa maana hila zao ni bure.
119 Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka, Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako.
120 ① Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.
121 Nimefanya hukumu na haki, Usiniache mikononi mwao wanaonionea.
122 ② Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema, Wenye kiburi wasinionee.
123 Macho yangu yanafifia kwa kuungojea wokovu wako, Na kutimizwa kwa ahadi yako ya haki.
124 Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe.
125 Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako.
126 Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako.
127 ③ Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.
128 Maana nayafuata mausia yako yote, kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.
129 Shuhuda zako ni za ajabu, Ndiyo maana roho yangu imezishika.
130 ④ Kufafanuliwa kwa maneno yako kunatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
131 Nafunua kinywa changu nikihema, Maana nazitamani amri zako.
132 ⑤ Unigeukie na kunirehemu, Kama ilivyo desturi yako kwa walipendalo jina lako.
133 ⑥ Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki.
134 ⑦ Unikomboe kutoka kwa dhuluma ya mwanadamu, Nipate kuyashika mausia yako.
135 ⑧ Umwangazie mtumishi wako uso wako, Na kunifundisha amri zako.
136 ⑩ Macho yangu yachuruzika mito ya machozi, Kwa sababu hawaitii sheria yako.
137 ⑪ Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki, Na hukumu zako ni za adili.
138 Umeziagiza shuhuda zako kwa haki, Na kwa uaminifu mwingi.
139 Juhudi yangu imeniangamiza, Maana watesi wangu wameyasahau maneno yako.
140 Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
141 ⑫ Mimi ni mdogo, nadharauliwa, Lakini siyasahau mausia yako.
142 ⑬ Haki yako ni haki ya milele, Na sheria yako ni kweli.
143 Taabu na dhiki zimenipata, Maagizo yako ni furaha yangu.
144 Haki ya shuhuda zako ni ya milele, Unifahamishe, nami nitaishi.
145 Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike; Nitazishika amri zako.
146 Nimekuita Wewe, uniokoe, Nami nitazishika shuhuda zako.
147 Naamka kabla ya mapambazuko na kukuomba msaada, Naweka tumaini langu katika maneno yako.
148 ⑭ Nakaa macho usiku kucha, Ili kuitafakari ahadi yako.
149 Kwa fadhili zako uisikie sauti yangu, Ee BWANA, uniokoe.
150 Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki, Wamekwenda mbali na sheria yako.
151 ⑮ Ee BWANA, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli.
152 ⑯ Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.
153 ⑰ Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako.
154 ⑱ Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako.
155 ⑲ Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako.
156 Ee BWANA, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako.
157 Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini mimi sikiuki shuhuda zako.
158 Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako.
159 Uangalie niyapendavyo mausia yako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako.
160 Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
161 ⑳ Wakuu wameniudhi bure, Ila moyo wangu unakaa kwa kicho cha maneno yako.
162 Naifurahia ahadi yako, Kama apataye mateka mengi.
163 Nimeuchukia uongo, umenikirihi, Sheria yako nimeipenda.
164 Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako.
165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
166 Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako, Na maagizo yako nimeyatenda.
167 Nafsi yangu imezishika shuhuda zako, Nami nazipenda mno.
168 Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako, Maana njia zangu zote ziko mbele zako.
169 Ee BWANA, kilio changu na kikufikie, Unifahamishe sawasawa na neno lako.
170 Dua yangu na ifike mbele zako, Uniponye sawasawa na ahadi yako.
171 Midomo yangu na itoe sifa, Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, Maana maagizo yako yote ni ya haki.
173 Mkono wako na uwe tayari kunisaidia, Maana nimeyachagua mausia yako.
174 Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, Na sheria yako ndiyo furaha yangu.
175 Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu, Na hukumu zako zinisaidie.
176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea; Umtafute mtumishi wako; Kwa maana sikuyasahau maagizo yako.
Leave a Reply