Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia bidii
Mithali 13 : 4
4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
Mithali 10 : 4
4 ⑩ Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Wagalatia 6 : 9
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
1 Wakorintho 15 : 58
58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Mithali 22 : 29
29 Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
2 Petro 3 : 14
14 ⑳ Kwa hiyo, wapenzi, mnapoyangojea mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane mkiwa na amani, bila doa wala dosari mbele yake.
2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Mithali 12 : 24
24 ⑥ Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.
2 Petro 1 : 10
10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
Mithali 11 : 27
27 Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia.
Yakobo 1 : 12
12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Mhubiri 9 : 10
10 Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Mithali 6 : 6 – 8
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
Kutoka 15 : 26
26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Wafilipi 3 : 14
14 nakaza mwendo, niifikie tuzo la thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
2 Mambo ya Nyakati 31 : 21
21 ⑧ Na katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu wake, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa.
Waraka kwa Waebrania 6 : 10 – 12
10 Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;
12 ili msiwe wavivu, bali mkawe kama hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.
2 Petro 1 : 5 – 7
5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo jitahidini sana ili katika imani yenu mtie na wema, na katika wema wenu maarifa,
6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu subira, na katika subira yenu utauwa,
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
Mithali 10 : 22
22 ⑲ Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.
Mithali 4 : 1 – 296
1 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.
3 Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 Usimwache, naye atakusitiri; Umpende, naye atakulinda.
7 Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji la uzuri.
10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.
14 Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya.
15 Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako.
16 Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
17 Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya ujeuri.
18 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
19 Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Jiepushe na kinywa cha ujeuri, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
27 Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.
Leave a Reply