Biblia inasema nini kuhusu Bethueli – Mistari yote ya Biblia kuhusu Bethueli

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bethueli

Mwanzo 22 : 23
23 Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu.

Mwanzo 24 : 15
15 ⑳ Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Abrahamu, naye ana mtungi begani pake.

Mwanzo 24 : 24
24 Akasema, Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, aliyemzalia Nahori.

Mwanzo 25 : 20
20 Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.

Mwanzo 28 : 2
2 Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.

Mwanzo 28 : 5
5 Basi Isaka akamtuma Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *