Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Barua
2 Samweli 11 : 14
14 Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu barua, akaituma kwa mkono wa Uria.
2 Wafalme 5 : 6
6 Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake.
Isaya 37 : 14
14 Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.
Isaya 39 : 1
1 Wakati huo Merodak-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa mgonjwa, na kwamba amepona.
2 Wafalme 19 : 14
14 Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.
Nehemia 2 : 9
9 Ndipo nikafika kwa watawala wa mkoa walio ng’ambo ya Mto, nikawapa nyaraka hizo za mfalme. Naye mfalme alikuwa ametuma maofisa wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami.
Nehemia 6 : 5
5 Ndipo Sanbalati akamtuma kwangu mtumishi wake vile vile mara ya tano, na barua wazi mkononi mwake;
Luka 1 : 4
4 upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Matendo 1 : 1
1 Kitabu kile cha kwanza nilikiandika, Theofilo, kuhusu mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha,
Matendo 23 : 30
30 Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na ghasia juu ya mtu huyu, mara nikamtuma kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.
Filemoni 1 : 25
25 Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.
2 Wakorintho 3 : 1
1 ② Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu?
Leave a Reply