Biblia inasema nini kuhusu Bahurim – Mistari yote ya Biblia kuhusu Bahurim

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bahurim

2 Samweli 3 : 16
16 Huyo mumewe akafuatana naye, huku akilia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.

2 Samweli 16 : 5
5 Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda.

2 Samweli 17 : 18
18 ⑦ Lakini kijana mmoja aliwaona, akamwambia Absalomu; basi wakaenda wote wawili kwa haraka, wakafika Bahurimu, nyumbani kwa mtu aliyekuwa na kisima uani mwake; wakashuka ndani yake.

2 Samweli 19 : 16
16 Akafanya haraka Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu akashuka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki mfalme Daudi.

1 Wafalme 2 : 8
8 ⑩ Hata, angalia, yuko pamoja nawe Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu, ndiye aliyenilaani kwa laana kuu siku ile nilipokwenda Mahanaimu; lakini akashuka kunilaki kule Yordani, nami nikamwapia kwa BWANA, nikamwambia, Mimi sitakuua kwa upanga.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *