Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Babeli
Yeremia 51 : 58
58 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia 50 : 1 – 46
1 ⑥ Neno hili ndilo alilosema BWANA, kuhusu Babeli na kuhusu Wakaldayo, kwa kinywa cha Yeremia, nabii.
2 ⑦ Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
3 ⑧ Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.
4 ⑩ Katika siku hizo, na wakati huo, asema BWANA, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta BWANA, Mungu wao.
5 ⑪ Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hadi kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
7 ⑫ Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.
8 ⑬ Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi.
9 Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.
10 ⑭ Nao Ukaldayo utakuwa mateka; wote wautekao watashiba, asema BWANA.
11 ⑮ Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;
12 mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika.
13 Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.
14 Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.
15 ⑯ Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.
16 ⑰ Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake.
17 ⑱ Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
18 Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, mimi nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
19 ⑲ Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi.
20 ⑳ Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala hakuna uovu; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.
21 Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.
22 Kuna kishindo cha vita katika nchi, Kishindo cha uharibifu mkuu.
23 Imekuwaje nyundo ya dunia yote Kukatiliwa mbali na kuvunjwa? Imekuwaje Babeli kuwa ukiwa Katikati ya mataifa?
24 Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
25 BWANA amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo.
26 Njooni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu chochote.
27 Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.
28 Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.
29 Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
30 Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA.
31 Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujia.
32 Na mwenye kiburi atajikwaa, na kuanguka, wala hapana atakayemwinua; nami nitawasha moto katika miji yake, nao utawala wote wamzungukao pande zote.
33 BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda wameonewa sana, na pia wana wa Yuda vivyo hivyo, watekaji wao wote wamewashikilia sana; na wamekataa kuwaachilia waondoke.
34 Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.
35 Upanga uko juu ya Wakaldayo, asema BWANA, na juu yao wakaao Babeli, na juu ya wakuu wake, na juu ya watu wake wenye hekima.
36 Upanga uko juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga uko juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika.
37 Upanga uko juu ya farasi wao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa.
38 Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.
39 Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwamwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hakuna mtu atakayekaa huko tangu kizazi hadi kizazi.
40 Kama vile ilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; kadhalika hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo.
41 Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.
42 Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.
43 Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
44 Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
45 Basi, lisikieni shauri la BWANA, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
46 Kwa kishindo cha kutwaliwa Babeli nchi itatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.
Ufunuo 17 : 1 – 18
1 ⑯ Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ⑰ ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 ⑱ Akanichukua katika Roho hadi jangwani, nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya kukufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 ⑲ Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 ⑳ Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.
7 Na yule malaika akaniambia, Kwa nini unastaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja itampasa kukaa muda mfupi.
11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye anaenda kwenye uharibifu.
12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.
16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.
17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.
Ufunuo 16 : 19
19 ⑬ Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
Ufunuo 18 : 1 – 24
1 Baada ya hayo niliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.
7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
8 Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.
9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;
10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.
11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;
12 bidhaa ya dhahabu, fedha, vito vyenye thamani, lulu, kitani nzuri, nguo ya rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, kila chombo cha pembe, kila chombo cha mti wa thamani nyingi, cha shaba, cha chuma na cha marimari;
13 na mdalasini, iliki, uvumba, marhamu, ubani, mvinyo, mafuta ya mzeituni, unga mzuri na ngano, ng’ombe na kondoo, farasi na magari, na miili na roho za wanadamu.
14 Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.
15 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza,
16 wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani, na lulu;
17 ① kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;
18 ② wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio kama mji huu mkubwa!
19 ③ Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.
20 ④ Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.
21 ⑤ Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.
22 ⑥ Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikika ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;⑦
23 ⑧ wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikika ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
24 ⑩ Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.
2 Wafalme 24 : 7
7 Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang’anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
Zaburi 137 : 8
8 ⑩ Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
Yeremia 32 : 28
28 Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitautia mji huu katika mikono ya Wakaldayo, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, naye atautwaa;
Yeremia 46 : 13 – 26
13 ⑰ Neno hili ndilo ambalo BWANA alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri.
14 Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote.
15 Mbona mashujaa wako wamechukuliwa mbali? Hawakusimama kwa sababu BWANA aliwafukuza.
16 ⑱ Aliwakwaza wengi, naam, wakaangukiana wao kwa wao; wakasema, Haya! Na tuondoke, tukarudi kwa watu wetu wenyewe, hadi nchi tuliyozaliwa, tuukimbie upanga unaotuonea.
17 Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muda alioandikiwa ameuacha upite.
18 ⑲ Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.
19 ⑳ Ee binti ukaaye katika Misri, Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa; Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa, Utateketezwa, usikaliwe na watu.
20 Misri ni mtamba mzuri sana, lakini uharibifu umekuja, Umekuja utokao pande za kaskazini.
21 Na askari wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama walionona malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikia, Wakati wa kujiliwa kwao.
22 Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu, Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni.
23 Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.
24 Binti ya Misri ataaibishwa; Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.
25 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;
26 nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.
Mwanzo 10 : 10
10 ⑪ Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
Danieli 3 : 1
1 ⑤ Nebukadneza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
Danieli 2 : 21 – 38
21 Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
22 yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.
23 Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.
24 Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonesha mfalme ile tafsiri.
25 Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri.
26 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake?
27 Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;
28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadneza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;
29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.
30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.
31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa la kutisha.
32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;
33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.
34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa joto; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.
37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
1 Petro 5 : 13
13 Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
Leave a Reply