Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Babeli
Mwanzo 10 : 10
10 ⑪ Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
Mwanzo 10 : 10
10 ⑪ Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
Mwanzo 11 : 2
2 ⑲ Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
Mwanzo 11 : 9
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Danieli 4 : 30
30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
2 Wafalme 25 : 13
13 ⑮ Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na vitako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 7
7 ③ Nebukadneza akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya BWANA mpaka Babeli, akavitia katika hekalu lake huko Babeli.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 10
10 ⑥ Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 18
18 ⑬ Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
2 Mambo ya Nyakati 36 : 20
20 ⑮ Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;
Isaya 45 : 2
2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma;
Yeremia 51 : 58
58 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia 51 : 44
44 Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
Yeremia 51 : 58
58 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Isaya 14 : 4
4 ⑫ utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi mdhalimu alivyokoma; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye ujeuri!
1 Petro 5 : 13
13 Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
Zaburi 87 : 4
4 Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi; Wanasema, Huyu alizaliwa humo.
Zaburi 137 : 9
9 Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.
Leave a Reply