Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia baba na watoto
Waefeso 6 : 4
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Malaki 4 : 6
6 ⑭ Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Waefeso 6 : 1
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
Wakolosai 3 : 21
21 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Leave a Reply